USIACHE MPAKA UONE MATOKEO
habari yako mwana wa mungu hongera kwa zawadi ya uhai uliopata leo, tumshukuru mungu kwa kusema asante kwa upendeleo huu kutoka kwa muumba.
leo ndugu yangu nipende kukumbusha kwenye makala hii kwamba USIACHE MPAKA UONE MATOKEO, kuna fulaha kwamba ya ushindi ipo siku utajitazama na kumshukuru mungu kwa maamuzi na ujasiri aliokupa kwa kutokuishia njiani.
yaweza kuwa upo ulipo hujui siku inaenda vipi una mbele wala nyuma huna nyumba wala ardhi kiufupi hauna chochote zaidi ya hizo ndoto zako, nachotaka kukuomba nikwamba usiachie njiani.
napoandika hili ni vile tu mimi nimechukua majukumu ya kuendelea kutokata tamaa lakini haimaanishi hakuna changamoto hata yule unayewaza kwenda kumuomba msaada sio kwamba hana pingamizi katika mambo yake bali ni maamuzi aliyoamua kusonga mbele.
kwahiyo kama unakata tamaa jiuliz tu kwanini ulianza na kwanini hutaki kuwa hapo ulipo kisha mshukuru mungu kwa hiyo changamoto kisha songa mbele maisha hayaitaji unyonge songa bila kusita.
nakutaki siku njema.!
Aidan Mponeza
Leave a Comment