HATUA KUMI YA KUBORESHA NGUVU BINAFSI ULIYOPEWA NA MUNGU


Rafiki wa mtandao wa fikia lengo na aidan mponeza hongera kwa siku nzuri ya leo maana hi indo mbegu ambayo inaweza kuotesha ndoto zako na zangu zikastawi vizur kwahiyo  tumshukuru mungu kwa hilo.

Rafiki naomba utambue  kwamba kila mmoja wetu hapa duniani anayo nguvu binafsi ndani yake ambayo ndio inaweza kumtofautisha na mwingine isingelikuwa huo ubinafsi alio nao kila mmoja wetu basi binadamu wote tungelifanana kwa kila kitu labda tunge tofautiana sura lakini ule ubinadamu tungekuwa sawa kwahiyo leo rafiki napenda kukushirikisha hatua kumi za kuboresha au kuibua nguvu binafsi uliyopewa na mungu.

  1. Tafuta sababu Zaidi kuliko kutafuta uhalisia;(NGUVU YA KIROHO).
       tafuta sababu wewe ni nani, unamtumikia nani, tafuta sababu kwanini umezaliwa Tanzania kwenye kutafuta sababu utapata chanzo cha jibu na hatua za kuchukua mfano tafuta sababu kwanini wewe ni maskini, kwanini unasomea hiyo taaluma, lakini ukitafuta uhalisia kwanini wewe ni maskini uhalisia utakujibu ni kweli wewe ni masikini lakini hautakupa sababu.
2
       2.Fanya machaguo kila siku;(NGUVU YA KUCHAGUA ).
       Rafiki naomba uelewe kwamba kuna machaguo ya aina mbili ambayo ni machaguo mabaya na machaguo ya aina mbili mfano kila shilingi  inayopita mkononi mwako inao uwezo wa kukuboresha kiuchui lakini unapokuwa na mia tano ukachagua kuinunua vocha kwa ajili ya kufatilia udaku wa mitandaoni jua umefanya machaguo mabaya.  Cha muhimu rafiki usijikute umefanya bali chagua kufanya.Chagua marafiki kwa uangalifu;(NGUVU YA USHIRIKIANO) .ni kweli dunia ya leo uwezo ukafanikiwa bila ushirikiano na wenye nguvu ya ushirikiano huo ni rafiki zako kama huna marafiki amua kuchagua leo na kuwa mwangarifu maana kikulacho kinguoni mwako.

                 4. Tambua kanuni itakayo kuongoza na jifunze kitu kipya;(NGUVU YA KUJIFUNZA HARAKA).
Ukweli ni kwamba kama maisha yako hayana kanuni utakuwa ni mtu wa kutakakujifunza kila linalokuja mbele yako na utachelewa kujifunza kwa sababu hauna kanuni ya kukuongoza lakini ukiwa na kanuni kila linalokuja utalipima na kanuni zako kama linastahili  ama lah.

                 5.  Jilipe mwenyewe kwanza.(NGUVU YA HESHIMA BINAFSI.)
 kuwa na uwezo wa kujilipa wewe kwanza kwa kila unalolifanya anza kwa kujilipa kuanzia muda wako kabla ujamlipa mwajili wako jilipe mwenyewe kipato chako kabla ya kuulipa mwili wako hii inakujengea kuwa na heshima binafsi juu ya kila kitu.

                   6. Walipe vizuri mawakala wako. (NGUVU YA USHAURI)
 Kwanza elewa kwamba kila mtu anae wakala kwa mfano wewe mwanafunzi wakala wako anaweza kuwa ni mwalimu wako nawe mwalimu wakala wako anaweza kuwa mwanafunzi wako, pia wale wenye familia wakala wako anaweza kuwa mkeo au mmeo pia hata watoto wako kwa wale wanaofanya biashara wakala wako ni huyo msaidizi wako kwenye biashara. Kwahiyo ndugu yangu jitaidi kuwalipa vizuri ili upate ushauri wowote kutoka kwao na elewa kwamba malipo sio lazima pes ahata utu wako na kuwapa muda wako ni malipo tosha.

               7. Toa Zaidi;(nguvu ya kupata kitu pasipo kuwa na kitu).
Ni ukweli kwamba ili upate laima utoe kwa mfano unaweza ukawa na taaluma juu ya jambo Fulani kwahiyo ili upate pesa nilazima  utoe hiyo taaluma Zaidi na mungu atakubaliki Zaidi kama ni mwalimu fundisha sana kama ni mshauri shauri sana.

                8. Tumia faida kuwekeza Zaidi na kununua hanasa(NGUVU YA LENGO LAKO).
     Ili kufikia lengo lako haupaswi mtaji ununue hanasa mfano moja ya mtaji wako ni mshahar uanaopata kwa vile mshahara ni kama mtaji tumia kuwekeza Zaidi na kamwe mshahara usinunue hanasa kama gari nguo a sikukuu nakazalika hii itakusaidia kufikia lengo lako.

                  9.  Chagua mashujaa wako;(NGUVU YA HADITHI).
Lazima uwe na shujaa wako ambao ndo watakua hadithi kubwa kwako hadithi ya safari zao  ndo zaweza kuwa mwanga wa kukuongoza katika safari yako kwa mfano kama unataka kuwa mwandishi wa hadithi shujaa wako anaweza kuwa shigongo elewa kunakili kutoka kwa shujaa wako ni njia ya kweli ya kujifunza.

                 10.   Fundisha na utapata;(NGUVU YA KUPATA).watu wapo tayari kupata kile ulichonacho kama ukiwafundisha na kama vina thamani wapo  tayari kukulipa kwahiyo usiwe na choyo toa elimu ya ulichonacho.

h    hizi ndo atua kumi za kuboresha kile ulichonacho ndani yako naomba tukutane tena kwenye makala inayofuata ni mimi mwandishi wako aidan mponeza.

mwandishi AIDAN MPONEZA
SIMU NO; 0762679204
EMAIL KWA USHAURI NA MAONIaidanmponeza@gmail.com
;


No comments

Powered by Blogger.