HII NDIO CHANGAMOTO KUBWA KULIKO ZOTE KWENYE MAISHA YAKO.



Ndugu yangu mpendwa wa mtandao wa fikia lengo, hongera kwa kupata zawadi ya siku ya leo ni jambo la kumshukuru mungu sana kwa kutuamini na siku ya leo kutupatia tena zawadi hii ya uzima.

Leo ndugu yangu nipende kukuuliza kwanini umepoteza mwelekeo, kwanini umeanza kuishi ovyo ovyo bila mikakati ya kuishi, kwanini unaanza kuwa na roho kukata tamaa, nakuuliza ndugu yangu kwanini umepunguza kujiamini kisa changamoto ndogo kama hizo, ndio.! Nasema ndogo maana changamoto kubwa ni moja tu duniani kukosa uhai.

Ndugu yangu haya yote unayopitia ni mapito yatapita ugumu unaopitia wewe leo mimi niliuona toka kitambo na ndio maana kwenye ukurasa wangu wa facebook nilikuambia ipo siku utabaki wewe na malengo yako basi.

Kuna muda ndugu yangu utaona wewe sio wa vile unavyotaka kuwa kuna muda hakuna wa kukupa msaada juu ya malengo yako Zaidi yaw ewe na malengo yako mwenyewe.

Nakuomba usipoteza mwelekeo, amini kule unataka kuwa ingali unapitia nyakati za kukukatisha tamaa, wewe usikate yamaa songa mbele song ahata kwa hatua ndogo lakini usipoteze mwelekeo.

Safari yako isisimame njiani yakupasa kusonga mbele bila Kurudi nyuma nakuomba usonge mbele ndugu yangu, songa,songa usipoteze mwelekeo nakutakia safari njema .

Unashauriwa kujaza taarifa zako katika fomu hapo juu ili upate Makala katika email yako moja kwa moja nakuwa miongoni mwa watu watakopokea zawadi ya kitabu kitakachotoka hivi karibuni asante sana.




instagram@Aidan_Mponeza
FACEBOOK@fikia lengo.
0762679204
email@aidanmponeza@gmail.com


No comments

Powered by Blogger.