UMUHIMU WA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI NA MAKINI;



Ndugu yangu kuna msemo unasema hapo ulipo ni matokeo ya maamuzi uliyofanya nyuma kwahiyo inaonyeha ni jinsi gani maamuzi yalivyo na umuhimu  katika maisha yetu na zifuatazo ni fanida ya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi.

KWANZA;inaboresha maisha yako, kiukweli ubora wa maisha yako ni matokeo ya maamuzi yako kwahiyo kama maisha yako ni bora basi maamuizi yako yalikuwa ni bora pia.

PILI;inahamsha umakini wa hisia ,unapofanya maamuzi kwa wakati sahihi unakua na hisia sahihi nakuziamini kwa maamuzi hayo.

TATu; inasaidia kumtafuta mungu katika hali, ni kweli unapokuwa mshindi wa kitu sifa ni kwake mungu na mafanikio ya maamuzi yako yanaweza kuwa ni chachu ya kuwa karibu na mungu.

NNE; inakupa uwezo wa kujiamini, uwezo wa kujiamini unatokana na maamuzi uliyofanya na unayoendelea kufanya kama maamuzi yako ni mabaya utapungukiwa na kujiamini mwenyewe nakuwa ni mtu wa kuomba ushauri kwa kila maamuzi yako hata yale maamuzi ya kawaida.

Tano,inakufanya uishi maisha yako ya ndani, unaweza kuwa na marafiki wengi ila mwenye uwezo wakufanya maamuzi yako ni wewe na unapofanya maamuzi unakuwa na hisia za ndani ndo zinakusukuma.

SITA; inaondoa kujilaumu katika maamuzi uliyofanya na kuwa na afya bora, kitendo cha kujilaumu tayari ni kujikataa na wewe na mwili wako na inaweza ikawa chanzo cha malazi kama moyo na mengine hakika maamuzi sahihi ni afya.

Ndugu hayo ndo muhimu na faida ya mafanikio lakini nikukumbushe ya kuwa maamuzi bora yanaitaji muda na gharama ya hali kama ikiwezekana na mali nikutakie siku njema na mungu akubariki karibu tena kwenye Makala zingine asante na AIDAN MPONEZA

 kama unaitaji ushauri  au maoni karibu sana kwa rafiki yako aidan tuma sms anza na neno FIKIA.
SIMU NO;0 762679204,
EMAIL; fikialengo@gmail.com
www.fikialengo.blospot.com


No comments

Powered by Blogger.