NCHI NZURI KULIKO ZOTE DUNIANI UNAYOPASWA KUISHI



Ndugu habari za uzima..!

Pole na majukumu ya leo na hongera kwa zawadi nzuri na kubwa uliyopepokea siku ya leo unaweza ukawa unajiuliza ni zawadi ipi hiyo.? Usiumize kichwa hakuna zawadi kama uhai duniani hapa ni jambo la kumshukuru mungu naomba nikutakie matumizi bora ya zawadi hiyo.

Ndugu yangu nchi ya Tanzania inawatu Zaidi ya milioni hamsini na kila mtu anaishi katika nchi yake kwahiyo kuna nchi Zaidi ya milioni hamsini ndani ya tanzania.

Yaweza kuwa nimekuchanganya kidogo lakini naomba unielewa kwamba nimezungumzia nchi kwa mtazamo wa uhuru na maisha unayoishi mtu binafsi kwa mfano wote mimi na wewe tunaishi Tanzania lakini uhuru tunatofautiana kwa mfano uhuru wa kifedha,kiroho, na hata utawala wa mtu binafsi ni tofauti sana ndio maana nimekuambia kuna nchi Zaidi ya milioni hamsini ndani ya tanzania.

Lakini ndani ya Tanzania kuna nchi unayostahili kuishi wewe hakuna nchi nzuri kama nchi unayofikiri wewe, na kama unapinga hili naomba abu fikiri kama watu wote Tanzania tukawa na utajiri  sawa wa kifedha hapo ndo utaona kila mtu akiishi kwenye nchi yake.

Jambo bora kabisa amua kuishi katika nchi unayoifikiri, nchi ya gari unalotaka kumiliki, nchi ya mke au mume unaemuitaji, nchi ya kiwango cha elimu unachokiitaji, nhi ya marafiki unaowaitaji nchi ya starehe unazoitaji na bahati nzuri ni kwamba nchi hii haipo mbali ipo katika fikra zako.

Nikukumbushe kwamba auwezi kwenda kwenye nje ya nchi pasipo kufuata taratibu halali za kuelekea nchi hiyo kwahiyo hivyo hivyo auwezi kwenda kuishi kwenye nchi hii pasipo  kufuata misingi ya kukufanikisha kufika nchi ya kufikirika. ni lazima uweke misingi madhubuti ya kukufikisha uko nakumbuka safari ya kilometa 100 uanza na mita moja, kwahiyo anza hapo ulipo kwa kile ulichonacho utafika.

Ni kukumbushe tu kwamba jitahidi ukiwa unaamka asubuhi unaamshwa na nchi hii ni nchi nzuri sana nakutakia siku njema usiache kujaza email yako katika mtandao huu na pia kulike ukurasa yetu ya fikia lengo facebook

Instagram@Aidan_Mponeza
facebook @page FIKIA LENGO
whatsapp no@0762679204
EMAIL@ aidanmponeza@gmail.com



No comments

Powered by Blogger.