BARUA YA WAZI KWA WATANZANIA JUU YA WASOMI WETU. 2017/2018



Ndugu yangu ni mimi mwandishi wako Aidan mponeza naandika barua hii kwa mapenzi ya dhati na taifa langu na kwa Imani yangu naomba iwafikie watanzania wote na wadau wa elimu ndani ya taifa hili. Kama walimu,wazazi,madaktari na maprofesa  na wengine wengi.
ndugu ni hali ya kufurahisha na kujipongeza kuona nchi yetu ilipofikia kwenye kiwango cha kuithamini elimu ni hatua kubwa ambayo ni ya kujisifia lakini pia  ni jambo la kujisifia taifa letu lilipo fikia kwenye kiwango cha wazalishaji wasomi wengi kutoka vyuo vikuu mbalimbali ndani na nje ya nchi ni jambo kubwa sana katika taifa.

Lakini pia jambo la kusikitisha ni kuona tunazalisha wasomi ambao ni tegemezi kwa jamii badala ya jamii kuwa tegemea wao hili ni tatizo katika taifa kama na mara nyingi tumekuwa tukirudisha mpira wa kona kwao wasomi hao kwamba tatizo ni lao mimi leo nataka kuwatetea juu ya swala hili.

Ni sahihi wasomi kuwalaumu kwa hatua wanayopitia baada ya kutoka vyuoni kwamba wao ndo tatizo hawachanganui akili zao lakini kuna tatizo ambalo lipo nyuma ya pazia ambalo tusipo litatua tutakua tumepata janga la kuzalisha wasomi waoga na wasiojiamini kwa kile walichosomea kuna ndugu yangu mmoja nilimueleza kwamba tatizo la wasomi wengi kutokujiamini linatoka katika jamii zetu kuanzia ngazi ya familia na akanibishia ila baada ya kumuelekeza akanielewa  vizuri sana.

Ukweli ni kwamba kama tukiendelea kuwashauri vijana wetu juu ya kitu ca kuwasomea na kuwaambia kwamba kasomee kitu fulan  tukubaliane na tatizo hili liendelee kutafuna taifa.

Ukweli ni kwamba thamani ya elimu leo inabadilika kwa kasi sana si muda wa kuipigia debe fani Fulani kwamba ni nzuri kwa ajira na kuwashauri vijana wetu kwenda kuisoma ni kuzalisha kundi la waoga wa kitu alichosemea maana utamshauri leo kwamba kasomee uandisi wa majengo kwamba ni mzuri lakini kuja akamaliza miaka mine ya usomi wake anakuta thamani ya uandisi wake umeisha hapo ndo anapunguza kutokujiamini juu ya alichosomea.

Ndugu yangu suluhisho la tatizo hili ni moja tu ili tuzalishe wasomi wanaojiamini tukubaliane kwamba ni lazima tubadilishe ufundi wa kushauri watoto juu ya elimu tunatakiwa kuwashauri watoto wetu kusoma wanachokipenda kwa dhati na pia kuwashauri wasomi wetu hasa wa vyuo vikuu kuwa wasome wanachokipenda na sio kisa baba upo kwenye nafasi Fulani unamshauri mwanao kasome kitu Fulani utambeba elewa moja kwa moja unampoteza mtoto huyo kabisa.
"soma unachokiamini na kukipenda upate kujiamini na kupenda ulichosomea"AIDAN MPONEZA

Elewa kuwa mtoto akisoma anacho kipenda atapata nguvu kubwa ya kukitetea kwa dhati maana kipo damuni kipo kwenye nafsi na ni tofauti na yule anaesoma kisa pesa hizo zilikuwa ni zama za nyuma maana utasoma kisa kazi yake inamshahara mkubwa je ukikosa kazi utapungukiwa hali ya kujiamini.

mwandishi AIDAN MPONEZA
simu no 0762679204kwa ushauri wowote juu kupitia mtandao huu BONYEZA HAPA
    


No comments

Powered by Blogger.