HII KWA AJIRI YAKO KIJANA WOSIA WA WAZEE SIO WAKUPUUZA.
Fikia.! Fikia.! Fikiaaa.! “babu anaita” naaaaam babu “fikia anaitika” njoo mjukuu wangu mwambie na dada yako lengo mje huku kilingeni “babu fikia anawaambia jukuu zake” sawa babu twaja tuje na mkeka.? Babu.”fikia na lengo wanauliza” njooni pia na kalamu na karatasi “babu fikia akiwaeleza wajuuku zake” sawa babu twaja. Baada ya fikia na lengo kufika mazungumzo yalikuwa hivi.!
BABU; wajukuu zangu leo nataka nena nanyi juu ya jambo moja maana mimi karibu mwili urudi mavumbini acha niwanenee yanayowapasa kabla ya mauti yangu khoooo.!khoooo.! “babu anakohoa”
FIKIA;babu pole sana lakini usiseme maneno hayo wewe bado tupo wote, eti LENGO “fikia akimuuliza dada yake lengo” ni kweli kaka babu mbona yupo fiti hata kukuzidi hahahhahahhaha “wakicheka”
BABU;wajukuu zangu leo naomba niwaulize swali alilo niuliza baba yangu kipindi na umri kama wenu wajukuu zangu naomba mniambie mkiwa watu wazima mnapendelea kuishi maisha gani.?
FIKIA; haaaa, babuu mimi napenda kuja kuwa tajiri na mwenye maisha mazuri sana.
LENGO; kwani maisha mazuri ni yapi kaka fikia.? Lengo anamuuliza kaka yake.
FIKIA; dada yangu LENGO maisha mazuri ni nyumba nzuri gari zuri na pesa nyingi.
LENGO; mmmmm kwani kwa akina aidan wanayo maisha mazuri maana nyumba yao nzuri na gari lao zuri.
FIKIA; Haaa.! Wale wanayo maisha mazuri si unaona shule wanayosomea, maisha mazuri yale dada yangu au naongopa babu.?
BABU; hahahahahhah.!mnanifurahisha sana wajukuu zangu na ndio sababu ya kuwaita hapa kilingeni kuwanenea yale yaliyo msingi wa maisha yenu ni kheri ukaijua kweli usiutumie lakini kuliko kutoijua kabisa , miaka 45 iliyopita nilikuwa na mawazo kama haya ya fikia kwamba maisha ni pesa,nyumba nzuri, na magari mazuri na kiukweli nilifanikiwa kutafuta hivyo na nikavipata japo nililala sana polini nili mwaga sana jasho na kukosana sana na wanaoijua kweli maana walinieleza kweli nikawachukia.
FIKIA;sasa babu maisha mazuri ni yapi.?
BABU;mjukuu wangu fikia na lengo kitu kizuri ni kile unachokipenda na kukiamini lakini kitu kizuri Zaidi ni kile kizuri kilicho kwenye Kusudi lako, msihangaike kutafuta pesa maana pesa haina undugu bali tafuta kipaji ulichonacho maana huyo ndo ndugu atakae kuletea pesa usitafute nyumba ya kukuifadhi bali tafuta njia ya kutatua matatizo ya watu na watu watakupa nyumba, gari unayotamani leo itaisha wakati lakini ukifanya ulichoumbiwa kitakuletea magari maana mwisho wake ni mwisho wako, wajukuu zangu kuweni na maarifa ya kuongoza mali zenu na jamii zenu na sio marafiki wakukusaidia katika mali zako.
LENGO;babu wewe ulifanya haya unayotueleza.?
BABU; wajukuu zangu miaka ya nyuma kulikuwa hakuna gari,nyumba nzuri na mtu mwenye pesa nyingi hapa mtaani kama mimi lakini niliambiwa kweli na wanayoijua kweli lakini sikuwaamini na hapo ndo nikaanza kutumia kweli nayoijua mimi na mwisho wa siku ni maisha haya ndo tafsiri ya kweli yangu wajukuu zangu maisha ya mafanikio yanazo kanuni zake wewe endelea kutembelea mtandao huu na kufata unayo elezwa utaijua kweli nahisi mtakuwa mmenielewa wajukuu zangu,
FIKIA;sawa babu ngoja tukaandae chakula cha jioni.(fikia na lengo wanaondoka),
BABU;sawa wajukuu zangu mungu awaongoze katika kuitambua kweli ya mafanikio kaeni karibu na Aidan hapahapa kilingeni. FIKIA LENGO.
www.fikialengo.blogspot.com
aidanmponeza@gmail.com
0762679204
aidanmponeza@gmail.com
0762679204
Leave a Comment