MAMBO NILIYOJIFUNZA KUTOKA KATIKA KITABU CHA MHUBIRI.




Katika kitabu cha biblia kuna vitabu vingi vya kujifunza katika Nyanja mbalimbali za maisha leo naomba nikushirikishe machache kati ya yale mengi nilio jifunza kutoka katika kitabu cha mhubiri ambae alikuwa ni mwana wa daudi ambae aliingia gharama katika kufanya uchunguzi katika maisha ya hapa duniani. Na haya ndo machache nilio jifunza kutoka kwa mwanafalsafa huyu wa yerusalemu.

1.kuwa na kiasi kwa yale yaliyopo duniani.

ukweli ni kwamba katika dunia hii kuna mengi sana ya kufanya mazuri na mabaya watu wengi hujikuta wakifanya yale ambayo ni mabaya kwa ajili ya kustarehesha nafsi zao mhubiri anatushauri kwamaba yote ni bure kabisa tunatakiwa kuwa na kiasi.

2.tunzo la jasho lako ni kufurahia kazi ya kile unachokitenda.unaweza ukawa unamwaga jasho lakini jasho lako halina tunzo hufurahii kile unachokifanya kwa mfano wewe ni mwajiliwa wa taasisis Fulani lakini kila siku unalalama juu ya kazi unayofanya ukweli ni kwamba unaukosea haki mwili wako.

3.hekima ni bora kuliko upumbavu.ukweli ni kwamba mwenye hekima anayo taa ya kumuongoza lakini mpumbavu yupo gizani haoni anapo elekea jitahidi kuwa na hekima na utoloke kwenye upumbavu japo mwisho wa yote ni mmoja.

4.hakuna chema kimfaacho mwanadamu Zaidi ya kula,kunywa na kufurahia kazi yake.
unaweza ukawa tajiri lakini hufurahii kazi yako basi maisha yako hayana maana hili nalo mwanafalsafa huyu ameona ni jambo la kushangaza kabisa.

5.kwa mwanadamu lipo jambo moja la kumfaa ambalo ni kufurahi na kujifurahisha muda wote aishipo duniani.
mwanadamu unapo kuwa duniani haina haja ya kuishi maisha ya pasipo furaha katika dunia hii haina haja ya kuwa mwenye huzuni duniani.

6.nguvu ya ushirikiano.
ni afadhari kuwa wawili kuliko kuwa peke yako , maana ikitokea mtu akaanguka mwenzake atamuinua lakini ole wake yule alie peke ake ni nani atakae muinua aangukapo.

7.mwanafalsafa huyu aligundua kwamba duniani mahali palipo na haki na uadilifu uovu unatawala.
8.wafu waliokwenda wasiporudi, wana nafuu Zaidi kuliko watu walio hai.
kwa sababu mhubiri ameona watu wanaokandamizwa hulia machozi lakini hakuna anaemfariji hili nalo ni jambo lakushangaza alilo liona mhubiri.

9.Ongezeko la mali huleta ongezeko ya walaji.
ndugu yangu nahisi unaweza kuwa shahidi katika swala la utumiaji wa pesa unavyokuwa na pesa matumizi yanaongezeka jitahidi uwe na kikomo cha utumiaji wa kipato maana walaji ni wengi kadri smali ziongezekapo


10.Ahidi kwa tahadhari.
kuwa amkini na ahadi na nadhiri unazoweka kama unaweka nadhiri jitahidi kutimiza kwa wakati maana ni afadhari kutoweka nadhiri kuliko kuweka nadhiri na usitimize . na kama uwezi kutumiza ahadi haina maana ya kuhaidi maana utapoteza huaminifu.

ndugu asante kwa kuwa mfatliliaji wa mtandao huu kwa ajili ya maarifa kila siku naomba tukutane kwenye makal inayo fuata ni mimi mwandishi wako AIDAN MPONEZA.

email kwa maoni na ushauri fikialengo@gmail.com
endelea kutembele mtandao huu wa www.fikialengo.blogspot.com

2 comments:

  1. Nimebarikiwa sana na mafunzo haya katika kitabu cha muhubiri.nakushauri kuwa unaweza ukawa unahusianisha ulichokielewa kutoka Kafka vitabu vingine pia ili tukuze uelewa zaidi

    ReplyDelete

Powered by Blogger.