VITU VYA KUZINGATIA UKIWA UNAOMBA MTAJI WA BIASHARA KUTOKA KWA MTU WAKO WA KARIBU(ndugu au rafiki).
Ndugu yangu karibu katika Makala ya leo ndani ya mtandao
wako pendwa wa FIKIALENGO kwa Makala ya leo
itakayoenda kukufikishia vitu vya kuzingatia kabla ya kuomba msaada wa mtaji kwa mtu wako wa karibu.
Siku ya leo nimekumbuka ule usemi unaosema ya kwamba mipango
bila pesa ni sawa na makelele, yaweza kuwa nawe ni miongioni wa wale watu wenye
malengo makubwa katika kufany biashara wenye wazo zuri la biashara lakini mpaka
sasa hawatekelezi sababu ya MTAJI.
Ndugu yangu rafiki yangu naomba nikuambie kwamba kupata
msaada wa kifedha kutoka kwa mtu hasa kama fedha ya mtaji inakupasa kutumia
Sanaa na mbinu ya uombaji na unatakiwa kuwa na utayari wa kutosa sana.
Zifuatazo ni vitu vya kuzingatia kabla ya kuanza kuomba
mtaji kwa mtu.
1.tambua biashara yako.(aina gani ya biashara unataka
kufanya).
Ni lazima ujue ni aina gani ya biashara unayotaka kufanya na
hiyo biashara inamvuto gani kwa yule unayetaka kumuomba msaada unajua unaweza
ukaenda kuomba msaada wa mtaji wa biashara ya kuuza kuku wakati unaemuomba
haamini kabisa katika hiyo biashara.
2.kiasi gani cha fedha utakacho omba.
2.kiasi gani cha fedha utakacho omba.
unajua unatakiwa kujua ni kiasi gani cha fedha unaitaji
matumizi ya hiyo fedha ni yapi ili kumtia hamasa unaemuomba sio unafika kwa muombwaji ndo
unaanza kupiga hesabu.
3.uhusiano baina yako na unaemuomba.
3.uhusiano baina yako na unaemuomba.
Unatakiwa kutambua vizuri uhusiano baina yako na mtoa msaada
hii itakulahisishia kutambua ni lugha gani ya ushawishi utakayo tumia na cha
msingi ni kwamba unatakiwa kujenga uhusiano huu muda mwingi kabla na sio
kipindi cha shida pekee.
4.amua mfumo utakao tumia kuomba msaada ni (moja kwa moja).
4.amua mfumo utakao tumia kuomba msaada ni (moja kwa moja).
Mfumo wa moja kwa moja ni mfumo ambao wewe unafika kwa mtoa msaada ukiwa hauna kitu
chochote Zaidi ya wazo lako la biashara
, lakini mfumo usio wa moja kwa moja ni ile hali ambayo muomba msaada kaanza
tayari biashara kidogo na anaitaji
mwendelezo.
5.unaamini vipi wazo lako.
5.unaamini vipi wazo lako.
Kitakacho fanya pia mtu akupe pesa yake ni wewe kutokana na
ujasiri ulionao juu ya kuimini biashara yako yaani mtu akikupa muda wa kuelezea
biashara yako ni kueleza wazo lako kwa kujiamini mpaka mtoa msaada aiamini
biashara yako pia.
6.mtoa msaada anakaa upande gani.
6.mtoa msaada anakaa upande gani.
Unatakiwa kumuonesha
mtoa msaada kwamba thamani yake inakaa upande gani wa kupata au
upande wa kukosa usimwambie tu mtu naomba pesa badae aelewi pesa yake inakaa upande
gani.
7.mfumo wa urejeshi.
7.mfumo wa urejeshi.
ni lazima umuonesha mtoa msaada kwamba unauhakika pesa yake itarudi kama anauitaji wa kutaka mrejesho wa pesa yake na inarudi kwa mfumo upi wa thamani au pesa mkononi .
8.Nidhamu ya pesa ya watu.
unatakiwa uwe na nidhamu ya pesa ya watu umeomba msaada wa mtaji pesa itumike kwa ajiri ya mtaji sio unapewa pesa ya mtaji inaanza kutumika kama pesa ya chakula au nauli kutoka pale ulipo pewa pesa hizo.
Ndugu yangu hivyo ndo vitu vya kuzingatia kabla ya kuomba
pesa ya msaada wa mtaji.
unashauriwa kujaza fomu kwenye mtandao huu ili kupata Makala hizi moja kwa moja kwenye email yako.
Aidan Mponeza
aidanmponeza@gmail.com
unashauriwa kujaza fomu kwenye mtandao huu ili kupata Makala hizi moja kwa moja kwenye email yako.
Aidan Mponeza
aidanmponeza@gmail.com
Leave a Comment