VITU VITATU VINAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUPATA CONNECTION.
Ndugu yangu mwanamafanikio hongera sana kwa zawadi ya siku
ya leo kutoka kwa muumba wetu maana hakuna zawadi iliyo kuu Zaidi ya uhai wako
maana uhai ndio kitu pekee kinachofanya usome Makala hii, kwahiyo ndugu yangu
hongera sana kwa zawadi ya leo.
Katika Makala ya leo nitakwenda kukuelekeza vitu vitatu
ambavyo vitakusaidia kupata connection katika fursa mbalimbali, nachokuomba ni
kuwa makini mwanzo a Makala hii mpaka mwisho.
Hatua ya kwanza;
KUJICONNECT.
Yaani hatua ya kwanza na ya msingi kuliko zote ni njia ya
kujikonnect na kule unakotaka kupata konection mfano unaweza ukawa unataka
kupata kazi katika ofisi Fulani jaribu
kujitolea kwenye ofisi hiyo yaani jaribu kujishusha sana ndugu yangu ili kupata unachokitaka kwa lugha
nyingine jipendekeze.
Hatua ya pili; FANYA KITU BORA BORA ZAIDI.
Unaweza ukajikonnect
lakini kama watu hawataona thamani yako ni lazima connection ipotee kwahiyo
jaribu kufanya kitu bora ili watu waone ubora wako na badae watakutengenezea connection sehemu
tofauti tofauti na maanisha ukipata naasi itumie vizuri zaidi.
Hatua ya tatu; fanya
bila kuchoka(kuwa na usugu).
Haijarishi unapata matokeo gani kwa muda huo unaotafuta connection, cha msingi wewe ni
kufanya mpaka uone matokeo yaani unafanya kazi mpaka unaowafanyia kazi wanaona
aibu na kukupa connection ya kile unachoitaji,
Asante sana rafiki yangu kwa kuwa nami katika Makala hii ya
leo tukutane katika Makala zingine, leo ni kuache na Hizo hatua ambazo unaweza kufata ukiwa unatafuta
connectio mbalimbali.
Nakushauri kujaza fomu iliyopo ndani ya fikia lengo kuweza
kutumiwa Makala moja kwa moja kwenye email yako.
Leave a Comment