BARUA YA WAZI KWA WANAFUNZI NA WAHITIMU WA MASOMO YA UALIMU SAYANSI PAMOJA NA HISABATI.
Ndugu yangu habari za
uzima, natumai upo salama na unaenderea na majukumu ya kupambana na kazi ya
kukufikisha kwenye ndoto zako.
Ndugu yangu nimeamua kuandika barua hii kwa wanafunzi pamoja
na wahitimu wa masomo ya ualimu sayansi
pamoja na hisabati, ili kuweka sawa mambo kadha wa kadha.
Ni ukweli usio itaji mjadala kwamba Tanzania ya viwanda
inaitaji wingi wa wataalamu wa sayansi katika sehemu tofauti tofauti, na ili
tupate wataalamu hao hakuna budi kuwaitaji walimu wa masomo hayo ya sayansi, kwahiyo
hizi na habari njema kwa wataaluma wa masomo hayo.
Lakini leo nimejikuta
naitafakari kwa kina fani hii kwa
miaka mitano iliyopita na kisha nikaitafakari kwa miaka mitatu ijayo nikagundua kwamba kadi miaka inavyo ongezeka fani hii inakuwa
na changamoto za kutosha.
Nikagundua kwamba moja ya changamoto miaka mitano iliyopita
kulikuwa na uhitaji wa walimu katika shule nyingi kutokana na sera ya nchi
kuanzisha shule kila kata kutokana na sera hiyo basi ikapaswa kuweka
hamasa kwa wanafunzi kwenda kusoma kozi
hiyo.
Lakini nikagundua kuwa baada ya miaka mitatu mbele kuna hali
ya hatari kwa wahitimu wa masomo hayo maana idadi yao imekuwa ni kubwa kuliko idadi ya
shule, sijasema kwamba shule haziitaji walimu wa masomo hayo hapana, bali na
maanisha kwamba ebu na wewe tafakari idadi ya wahitimu wanaomaliza na
wanaoendelea kusomea na waliokwisha maliza na idadi za shule utaelewa na
maanisha niini.
Kwahiyo ndugu yangu mhitimu huu si muda wa kusubiri ajira si
muda wakujipa tumaini kwamba mwaka ujao utaajiriwa maana kila mwaka kuna idadi
ya wahitimu wengi mtaani kwahiyo wewe
kusubiri miaka miwili ya ajira ni mara mia ungelianza kufuga kuku wawili kwa
miaka miwili ungelikuwa ni mtaalamu wa kuku na ungelikuwa unajipatia kipato.
Kalamu naweka chini kwa kuhitimisha baua hii kwa kukuambia
kwamba kama upo mtaani ebu toa mawazo kuhusu ajira kutoka serikalini kwanza, na
kama upo shule ebu fikiria na kuhusu mtaani na baada ya hapo panga malengo yako
na mikakati ya kuifikia kule unakotaka
kufika.
Asante sana kwa kusoma baua
hii nakukaribisha kwa maoni ushaui na changamoto inayokukabili nitumie
email name nitakushauri.
Karibu sana
Leave a Comment