NI KWELI KABISA UNAYO MALENGO NA MIPANGO LAKINI HAUTAWEZA KUFIKIA SABABU UTEKELEZI HILI.



Ndugu habari……!

Ndugu yangu karibu katika Mtandao wa fikia lengo kwa lengo kuu moja kupata maarifa na kuyatumia katika safari yako ya mafanikio.

Ndugu yangu hivi ulishawahi kujiuliza tangu umezaliwa ulishakutana na watu wangapi ambao hawataki mafanikio na wangapi wanataka mafanikio katika maisha yao, kiukweli hakuna asiyetaka mafanikio katika hii dunia.

Lakini pia ulishawahi kusikia malengo na mipango ya wangapi, kiukweli binadamu wengi tunamipango mingi na malengo mazuri san ahata wewe ndugu yangu unaye soma hapa yaweza kuwa unayo malengo na mipango safi kabisa na hiyo ndo tofauti ya binadamu na wanyama.

Lakini swali la kujiuliza kwanini watu hawafanikiwi kwenye malengo yao, hivi ndugu yangu ushajiuliza hili swali kwanini inakuwa ngumu watu kufanikiwa kule walipo panga kufika. ?

Ndugu yangu wewe unaesoma hapa sasa hivi unaweza ukawa umeweka malengo na mipango lakini kama hautaweza kuamua kuishi mipango na malengo yako basi utaweza kufika popote.

Naposema kuishi mipango na malengo yako katika maisha na maana kwamba kwenye shuguli zako za kila siku asilimia 70 ya shughuli zako ni lazima ziwe zinagusa malengo yako kwa namna yoyote hili.

kwahiyo kabla ujafanya chochote kikubwa kabla siku yako haijaisha jiulize umeyagusa malengo yako kwa kiwango gani siku ya leo.? umetekeleza lipi litakalo sogeze maisha malengo yako au ndo wale wakutuambia kila siku nitafanya nitafanya sasa ndo muda huu fanya ishi malengo yako.

unachokosea ni kwamba kwa mfano wewe unaesoma hapa si unayo malengo ya kufikia kiwango Fulani cha kifedha sasa inapopita wiki moja au mbili bila kuhifadhi au kuwekeza kwenye kipato chako utakuwa umekwama kufika unakotaka.

Kwahiyo ndugu yangu hata kama uwe na malengo ya kutisha kiasi gani lakini kama hauta ishi malengo na mipango yako basi unakazi ngumu sana na unatakiwa kuniona tushauriane nini cha kufanya usiwe na shaka tutasaidiana wasiliana nami email hapa.

Na nikukumbushe tu kwamba kama bado ujajiunga na mtandao huu kwa njia ya email ili kuweza kupata Makala hizi moja kwa moja kwenye meail yako unaweza kufaya hivyo kwa kujaza taarifa zako katika mtandao huu.

Imeandikwa na AIDAN MPONEZA
EMAIL.aidanmponeza@gmail.com


No comments

Powered by Blogger.