HUYU NDO ADUI MKUBWA WA KUJIAMINI KWAKO.



Ndugu yangu hongera sana kwa siku ya leo hii ndio fursa pekee ambayo inaweza kukufanikisha kufikia malengo yako maana hakuna fursa iliyokuu Zaidi ya fursa ya uhai.

Uwezi kufika malengo yako kama aujiamini na kwa sababu hiyo leo mtandao wa fikia lengo umekuletea Makala itakayokuonesha adui mkubwa wa kujiamini kwako kabla sijaendelea na Makala hii nakushauri kuwa mwanachama wa mtandao huu kwa kujiunga kupitia fomu iliopo katika mtandao huu.

Ndugu yangu uwezi kufanikiwa kama unao uwezo mdogo wa kujiamini maana kama haujiamini auwezi kufanya vitu vikubwa vilivyo juu ya uwezo wako.

Na kwa kawaida malengo yako makubwa kwa sasa yapo juu ya uwezo wako na ndio maana unayafukuzia kuyashika  kwahiyo kama haujiamini basi upo kwenye hatari kubwa ya kutokutimiza malengo yako.

Lakini ndugu yangu kama ulishawahi kutokewa na hali ya kutojiamini juu ya kutekeleza jambo Fulani basi kuna adui mkubwa anae fanya zoezi hilo.

Ndugu yangu hakuna adui mkubwa wa kujiamini kwako kama hofu, hofu ndo adui anaekuambia uwezi pale unapoona ya kuwa unaweza, hofu ndo adui anae kupa majibu hasi kabla hata ujafanya jambo Fulani.

Namna moja tu ya kumpinga adui hofu kwanza ni kutokumsikiliza sababu zake maana sababu nyingi uwa ni za uongo unaweza ukawa unataka kufika ofisi Fulani ukikaribia mlangoni utasikia hofu anakupa sabab ya kutosafisha kiatu kuna nafsi utasikia ikisema “TAZAMA KIATU KILIVYO KICHAFU”  huyo ndo adui hofu.

Lakini pia unaweza kumuepuka adui hofu na kuongeza uwezo mkubwa ya kujiamini kwa kufanya maandalizi mazuri kabla ya tukio, maandalizi humkimbiza hofu maana unakuwa umevunja sababu ambazo adui hofu uzitoa.

Ndugu yangu kwa leo mwandishi wako AIDAN MPONEZA naomba niishie hapo tukutane kwenye Makala nyingine ndani ya mtandao huu lakini pia katika mitandao yangu ya kijamii facebook page(FIKIA LENGO)
instagram@aidan_mponeza. Asante sana nakutakia mafanikio mema kwenye kazi zako.

Aidan Mponeza
email@aidanmponeza@gmail.com



No comments

Powered by Blogger.