CHOCHOTE UNACHOKIFANYA UNAKIFANYA KWA HISIA HIZI.
Ndugu yangu habari za uzima.!
Kama kuna zawadi ambayo unastahili sana kujivunia kuwa nayo
ni pamoja na zawadi ya siku ya leo hakuna zawadi kama hii maana msingi wa
mafanikio yako yote yanatokana na siku hii ya leo kiukweli ni jambo la
kumshukuru mungu.
Ndugu yangu karibu katika Makala ya leo ambayo itakwenda
kueleza ni hisia zipi zinazo mfanya mtu kufanya kitendo chochote katika maisha
yake, na kati ya hisia hizo ni ipi ni hisia sahihi kutumia.?
Ndugu yangu kama unafanya jambo lolote katika maisha yako
basi elewa unafanya jambo hilo ukiongozwa na hisia kuu mbili katika kutimiza
kufanya jambo hilo, zifuatazo ni hisia mtu atumiazo kufanya jambo au kitendo
chochote chenye matokeo katika maisha yake.
Kwanza(HISIA YA HOFU); hofu ni moja ya hisia ambazo upelekea
mtu kufanya jambo Fulani kwa mfano unaweza kutoa mchango Fulani labda wa harusi
au msiba kwa kuhofia kuchekwa au kutengwa, na pia hisia hii ya hofu ndo
inayopelekea mtu kutekeleza sheria zilizowekwa kwa kuhofia kukumbwa na adhabu kwa
kukeuka sheria hizo. lakini sio kila tendo linafanywa kwa hisia hii ya hofu
hapana.
Pili(HISIA YA MATAMANIO);
hisia ya matamanio ni miongoni mwa hisia ambazo umtawala mtu katika kutekeleza
jambo Fulani, mfano kama wewe unandoto za kuwa miongoni mwa mamilionea ndani ya
nchi hii kwahiyo itakuitaji uwekeze, kitendo cha wewe kuwekeza uletwa na hisia
tosha za matamanio ya kufika kule unataka.
JE IPI NI HISIA
SAHIHI KUTUMIA; kiukweli ni kwamba hisia zote hizi mbili ni nzuri kutumia
kutokana na jambo unalofanya lakini katika safari yako ya mafanikio ni vizuri
ukatumia hisia ya matamanio Zaidi kuliko kutumia hisia ya hofu kwa maana kwamba
hisia ya hofu uzalisha uwoga juu ya jambo ambalo unataraji kutekeleza sasa hii
ni hatari kama hisia ya hofu ikikuzidia maana uwoga ni chanzo cha
kutokujiamini.
Lakini ili ufike ni lazima utumie hisia zote hizi, ni
lazima uwe na hisia ya matamanio makubwa ya kufika kule unataka na ni lazima
pia uwe na hofu ya kupoteza kile ulichokipata ili uweze kufika salama.
Asante sana kwa Makala hii ya leo usiache kujaza taarifa
katika mtandao huu ili uweze kupata Makala hizi moja kwa moja kwenye email
yako.
Aidan Mponeza
0762679204
0762679204
Leave a Comment